Monday, 16 September 2013

KAMA ULIKUWA HUJUI,BASI HIKI NDICHO WCB TULICHOKIFANYA FIESTA MOROGORO USIKU WA JANA




Msimu wa Fiesta 2013,unaendelea na jana ilikuwa ni zamu ya
 watu wa Morogoro kupewa burudani harisi kutoka kwa watoto wa kitanzania,mimi na Crew yangu ya WCB tuliwasili Morogoro mapema mchana na kuungana 
na wasanii wenzangu,waliokuwa wameshatangulia.Kiukweli sitochoka
 kuwashukuru mashabiki wangu wa Moro kwa sapoti na mapenzi makubwa
 waliyoyaonyesha on stage,hawakuniangusha
 na hii inazidi kunipa deni la kuaandaa mambo mapya na mazuri zaidi kwa ajili yenu ..nisiongee sana,nakuachia picha ziongee zenyewe!!!

Baada ya kuwasili eneo la tukio,nikisalimiana na baadhi ya wasanii waliokuwa wametangulia..
mmh Recho kunitoleaa macho!!Linah anachekelea tu kwa mbali

Rommy Jones na Shadee wa Clouds

My boy Qboy msafi akifuatilia kitu kwa makini

Kwanza tukaanza kuwalewesha kwanza kama hivi..........



Hilo nyomi sasa..watu wangu wa Moro mlitisha saaana!!!





Ama nini...!!


Hapa ni mwendo wa kuimba wote tu



My boy Dummy

Rommy J on one&two


Noma sana...







Nikiitazama moja ya siraha yangu ya WCB,Imma pltnumz anavyowatendea haki mashabiki

Tulia bwana mdogo hebu nitizame mimi kwanza


Dummy







Ikafika ile time ya kumkalisha huyu bitozi wa Manzese




Brothermen vipi bado unabisha??

Ubaya  wenu wengi kayumba,elimu mliitupa sandakalawe!!!!

Dada zetu wanavaaga nguo za hivi kweli??huyu Nay vipi!!!


Bora nikimbie usije nipiga mbata..ha ah ah a..was so fun




Twangala Dozen &Fetty 


They call him Kiroboto the legendally,alikuwepo pia

Monday, 9 September 2013

GAREHT BALE ABURUZWA VIBAYA NA MESUT OZIL KATIKA MAUZO YA JEZI



Ozil ArsenalOzil Arsenal
Gareth Bale anaweza kuendelea kupokea maneno yasiyo ridhisha kwa kumbadili  Mesut Ozil katika klabu ya Real Madrid baada ya wauzaji wakubwa wa jezi za soka mtandaoni UKSoccershop.com kuthibitisha kwamba mauzo ya jezi za nyota mpya wa Arsenal yameyazidi yale ya Bale kwa kiwango kikubwa.

Madrid tayari wamekuwa katika hali ngumukwa kumruhusu Ozil kuondoka kwa ada ya uhamisho ambayo walilipa kwa Bale - hivyo kumfanya mchezaji huyo wa Wales kuwa mchezaji ghali zaidi duniani kwa ada ya uhamisho wa £86million.

Presha kubwa sasa ipo kwa Bale kuelekea mchezo wake wa kwanza na Real Madrid wikiendi ijayo, huku sasa namba za mauzo ya jezi zikionyesha kwamba ni mchezaji aliyembadili ndani ya kikosi cha Carlo Ancelotti ambaye ameshika usukani kwa kuuza jezi nyingi. 


Mkurugenzi wa UKSoccershop.com Simon Pretswell alisema: 'Ukiachana na masuala ya uwanjani, sehemu kubwa ya uhamisho ghali duniani huwa umetaliwa na sababu za kibiashara zinazokuja na ukubwa wa mchezaji husika.'
'Katika kesi ya Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na mastaa wengine wa zamani kama David Beckham, hawa walileta fedha nyingi kwa klabu kwa mauzo ya jezi kupanda kwa kiasi kikubwa.'

Gareth Bale ameshindwa kuleta mauzo makubwa ya jezi kama ilivyo kwa Mesut Ozil na Neymar walipohamia kwenye vilabu vyao vipya katika dirisha hili la usajili.' 
'Kipaji cha Bale hakina mashaka, lakini hajawahi kuwa mmoja ya wauzaji wakubwa wa jezi katika premier league, huku mashabiki wakivutiwa zaidi na jezi za Wayne Rooney, Robin van Persie, Steven Gerrard na even Fernando Torres.'

Jack Wolper awataka wasanii wa kike WAJIHESHIMU kwa kutovaa mavazi ya nusu UCHI


.


Muigizaji wa filamu za  kibongo  maarufu  kwa  jina  Jackline Wolper amewaasa waigizaji wenzake wa kike kuacha kuvaa nguo za nusu uchi kwani ni kinyume na mila na tamaduni za kitanzania .

Wolper aliyasema hayo kufuatia kupigiwa kura na kushinda kama muigizaji wa kike mwenye muonekano wa kistaa...

Akizungumza katika kipindi cha filamu cha Take One kinachorushwa Clouds Tv , Wolper alisemakuwa  yeye hawezi kuvaa mavazi ya nusu uchi ila anavaa  mavazi yanayomsitiri mwili wake na bado anapendeza kuliko hao wanaovaa nusu uchi halafu hawapendezi.

"Nawashukuru  sana mashabiki wangu kwa kunipigia kura hadi kuibuka mshindi, na ni kweli najiamini kwa kuwa mimi hata siku moja huwezi kuniona nimevaa nguo za nusu uchi kama wengine" Wolper

IFUATAYO NDIYO LIST YA MASTAA 10 WANAOLIPWA MSHIKO MREFU HOLLYWOOD



Kwa mujibu wa Jarida na kampuni inayojishugulika na maswala
ya utafiti wa kuangalia maendeleo
na vipato vya wasanii,waigizaji na watu maarufu dunia,FORBES,hii ndio list
ya wacheza filamu nchini Marekani toka Hollywood
wanaoongoza kuwa na mshiko
mrefu zaidi Duniani.......



NIMEKUPANGIA LIST HII KWA MAJINA NA PESA WANAZOINGIZA:

1:Robert Downey Jr-IRON MAN (75 million$)

2:Channing Tattun-MAGIC MIKE,WHITE HOUSE DOWN(60 million$)

3:Hugh Jackmann-LES MISARABLE,XMAN(55 million$)

4:Mark Walhberg-TED(52 million$)

5:Dwayne 'The Rock' Johnson-Fast & Furious(42 million$)

6:Leonardo DiCaprio-Great Gatsby(39 million$)

7:Adam Sandler-Hotel Transylvania(37 million$)

8:Tom Cruise-Jack Reacher(35 million$)

9:Denzel Washington-Flight(33 million$)

10:Liam Neeson-Taken 2,The Grey(32 million$)