Habari
zilizo tufikia hivi punde katika meza yetu ya habari ya , zinapasha
kuwa Sheikh Ponda Issa Ponda anadaiwa kujeruhiwa na Polisi muda mfupi
baada ya kumaliza mhadhara wake Mjini Morogoro katika jaribio la
kumkamata.
Taarifa
kutoka eeo la tukio zinapasha kuwa Sheikh Ponda amejeruhiwa na bomu la
machozi lililoplipuliwa katika gari lake wakati wa jaribio hilo la
kumkamata jioni ya leo na kuzua mtafaruku mkali.
Aidha
taarifa hizo zinasema mara baada ya tukio hilo baadhi ya Mashekh
walimshusha katika gari lake na kumpakia katika Pikipiki na kumkimbiza
Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu lakini ghafla walibaini kuwa
Polisi wanawafuatilia na kuamua kuingia hospitalini hapo na kutokea
mlango wa uwani na kutokomea.
Mtoa
taarifa mjini Morogoro anapasha kuwa wakati Ponda akitoroshwa mikononi
mwa Polisi mlango wa uwani Polisi walitinga Hospitalini humo kufanya
msako wa Shekh huyo ambaye amekuwa akileta kizazaa zaa kutoka na
mawaidha yake na msimamo wake wa utetezi wa mali za Waislamu nchini.
Taarifa kamili ya tukio hilo itakujia wakati wowote kuanzia sasa endelea kuifuatilia.
0 comments:
Post a Comment