![]() |
Rais wa Rwanda Paul Kagame |
Katika
hali inayoonyesha serikali ya Rwanda sasa imeshtushwa na hotuba kali ya
Rais Kikwete aliyoitoa hivi karibuni na kuzungumzia kauli za Rwanda za
kumtukana, kwa mara ya kwanza serikali ya Rwanda imetoaa tamko
linaloonyesha kuwa nchi hiyo imeanza kuwa na tahadhari katika kujibu
masuala yanayomhusu Rais Kikwete.
Rwanda
kupitia waziri wake wa Mambo ya Nuje, Louise Mushikiwabo, ilikaririwa
ikieleza kwamba hawatajibu mapigo agizo la Rais Jakaya Kikwete ya
kuwataka Wanyarwanda wote waliolowea Magharibi mwa Tanzania kuondoka
haraka.
“Ni
uamuzi ambao umeshachukuliwa, hatukushirikishwa kwa namna yoyote na
jukumu letu kama serikali na taifa ni kuwahakikishia ulinzi wote
wanaokuja, na hili ndilo suala tunalolishughulikia kwa sasa,” alisema.
Kwa
mujibu wa gazeti la New Times, Mushikiwabo aliwaeleza waandishi wa
habari kwamba agizo hilo la Rais Kikwete pamoja na ushauri wa kuitaka
Serikali ya Rwanda kuzungumza na wanamgambo hasimu wa FDLR waliopo
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), hayatayumbisha uhusiano imara
baina ya Watanzania na Wanyarwanda.
“Sisi
si majirani tu, tuna mfungamano imara baina ya watu wetu pia, tuna
mfungamano wa damu, wa kibiashara, na mengine mengi ya kutufanya
tuendelee kuwa pamoja,” alisema na kutumia fursa hiyo kuwakaribisha
Watanzania nchini Rwanda.
Watanzania
wanaweza kuishi hapa kwa umri wowote wanaotaka. Tunawachukulia kuwa ni
watu wetu muhimu kwenye fungamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki,”
alisisitiza.
Rais
Kikwete wakati akihitimisha ziara yake mkoani Kagera alitoa agizo la
kuwataka wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na wahamiaji haramu ama
kuondoka au kuhalalisha ukazi wao, huku akitoa wiki mbili kwa zoezi hilo
kutekelezwa, kabla ya kuanza kwa operesheni ya kuwasaka watu hao.
Kauli
hiyo ilitokana na kushamiri vitendo vya kihalifu katika eneo la Kanda
ya Ziwa, Rais hakutaja jina la nchi ya wahamiaji hao. Kwa ukanda huo
Tanzania inapakana na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC.
Pia,
Rais Kikwete katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi alizungumzia
kusikitishwa na kauli za shutuma, kejeli na udhalilishaji zilizotolewa
na Rais Paul Kagame wa Rwanda dhidi yake.
Mvutano
baina ya Rwanda na Tanzania ulianza kuwekwa hadharani Mei mwaka huu,
baada ya Rais Kikwete kuishauri Rwanda kukaa na kuzungumza na FDLR wenye
makao yao DRC, hatua ambayo haikuifurahisha Serikali ya Rwanda.
Wakati
Rwanda ikieleza hayo jana Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue
alizungumza na gazeti hili, na kutaka majibu ya kauli hiyo ya Rwanda
yatolewe na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
0 comments:
Post a Comment